Rais Joe Biden anataka kufufua juhudi zake za kuchaguliwa tena Jumapili, wakati wanachama wa chama chake wakijadili mustakabali wa kugombea kwake.
Utendaji wa rais katika mjdala wa urais wa wiki jana ulizua maswali mazito kuhusu uwezo wake wa kimwili na kiakili kugombea.
Mahojiano na chombo cha habari cha ABC siku ya Ijumaa yalichochea uvumi zaidi kuhusu mustakabali wa kampeni yake.
Katikati ya switofahamu hiyo, Bw Biden alionekana kwenye hafla mbili za kampeni huko Pennsylvania, jimbo kuuambalo linaweza likaelekea kwa mgombea yeyote Jumapili.
Lakini juhudi hizo hazijawazuia Wanademokrat wenzake kupima hatari na umuhimu wa kumweka Bw Biden, 81, katika tiketi kuu ya chama hicho.
Siku ya Jumapili alasiri, kiongozi wa walio wachache katika Baraza la Wawakilishi Hakeem Jeffries aliitisha mkutano na wabunge waandamizi katika chama cha Democratic ambao uliripotiwa kujumuisha mjadala wa ugombeaji wa Bw Biden.
Wanne kati ya waliokuwa kwenye simu hiyo walisema walidhani Biden anafaa kuacha kuwania, kulingana na CBS, mshirika wa BBC wa Marekani.
Vyanzo vilisema angalau wengine watatu walionyesha wasiwasi juu ya nafasi yake mnamo Novemba.
Baadhi ya viongozi wakuu wa Demokrats pia walitoa msimamo wao katika mahojiano ya televisheni mwishoni mwa juma, wakilenga kushughulikia swali: Je ni hatari zaidi kuendelea na Bwana Biden au kumuondoa?
Wengine wanasema chama kinaweza kushindwa dhidi ya Donald Trump mnamo Novemba ikiwa Bw Biden atasalia, lakini wengine wanasema kuondolewa kwake kutaleta mambo mengi yasiyojulikana.
Pia unaweza kusoma
Wengine wanaona fursa ya mwanzo mpya
Kuondoka kwa Biden aliyefanya vibaya katika mjadala wa urais dhidi ya Trump kunaweza kuleta ahueni ya haraka.
Baadhi ya Wanademokrasia, ikiwa ni pamoja na wafuasi wa rais, wamesema mengi, wakidai kwamba wasiwasi juu ya umri wake na akili yake umezua mjadala mgumu.
Mjadala huo "uliibua maswali kwa raia wengi wa Marekani iwapo rais ana nguvu za kumshinda Donald Trump", alisema Mwakilishi wa California Adam Schiff siku ya Jumapili.
Bw Schiff alishindwa kusema kuwa Biden anapaswa kuacha katika mahojiano yake na NBC News - msimamo ambao umechukuliwa hadharani na Wanademokrasia watano hadi sasa.
Badala yake, Bw Schiff alimtaka atafute ushauri kutoka kwa watu walio na "umbali na malengo" na kufanya uamuzi kuhusu ikiwa anaamini kuwa yeye ndiye mgombea bora zaidi.
"Kwa kuzingatia rekodi nzuri ya Joe Biden, ikizingatiwa rekodi mbaya ya Donald Trump, [Biden] anapaswa kumshinda Donald Trump, kwa wingi wa kura" Bw Schiff alisema. "Hapaswi kuwa karibu naye kwa sababu ya umri".
Bw Biden ana umri wa miaka 81, huku Trump akiwa ametimiza umri wa miaka 78. Umri wa wagombea wote wawili umekuwa suala linalozidi kuwa na utata miongoni mwa wapiga kura.
Upande wa kushoto, kura za maoni zinaonyesha baadhi ya wapiga kura wanapoteza imani na Bw Biden. Katika kura ya maoni ya Wall Street Journal iliyotolewa Ijumaa, 86% ya Wanademokrasia walisema watamuunga mkono Bw Biden, kutoka asilimia 93 mwezi Februari.
Mgombea tofauti pia anaweza kuonekana mtu mpya katika maeneo mengine, pia. Kabla ya wimbi hili la hofu ya Kidemokrasia, Bw Biden alikosolewa na wapiga kura katika nyanja kadhaa za sera, ikiwa ni pamoja na jinsi anavyoshughulikia uchumi wa Marekani na mzozo wa wahamiaji katika mpaka wa kusini mwa nchi hiyo.
Rais anakabiliwa na tishio kutoka kwa wapiga kura wanaopinga majibu yake kwa vita vya Israel huko Gaza.
Upinzani wao ulimgharimu zaidi ya kura 100,000 huko Michigan - jimbo muhimu sana - wakati wa mchujo mwezi Februari.
Tikiti ya Biden "itamrudisha nyuma kila mtu", alisema Mwakilishi wa zamani wa Ohio Tim Ryan Jumapili katika mahojiano na Fox News.
"Nadhani utaona shinikizo kubwa iwe leo au kesho, wakati fulani wiki hii, wanachama wanaporudi kwamba hii inaweza kuwa ngumu kwao."
Wengine wanasema kitakachojiri ni hatari kubwa
Faida yoyote ya kumpoteza Bw Biden inaweza kunyamazishwa na hatari zinazokuja, kulingana na viongozi wengine wa Democrats.
Ikiwa rais angesimama kando, mengi ya yale yanayojiri baadaye hayajulikani: ni nani angechukua nafasi ya Bw Biden, na vipi? Na mgombea huyo angeweza vipi dhidi ya Trump?
Na katika siku za hivi majuzi, washirika kadhaa wa Biden wamesisitiza kuhusu mitego ya kupanga upya, wakisema kwamba Bwana Biden amekuwa mafanikio yaliyothibitishwa.
"Biden ni mzee," Seneta wa Vermont Bernie Sanders, 82, alisema Jumapili kwenye CBS News. "Yeye sio mzungumzaji kama alivyokuwa hapo awali. Natamani angeruka hatua kwenye Air Force One. Lakini Hawezi. Tunachopaswa kuzingatia ni sera - sera zake zinanufaisha idadi kubwa ya watu katika nchi hii."
Gavana wa California Gavin Newsom, alisema vivyo hivyo katika mkutano wa hadhara huko Doylestown, Pennsylvania siku ya Jumamosi.
"Ni suala ambalo linazuia maendeleo katika kumkuza mgombea huyu," Bw Newsom alisema. "Hapa ndipo ambapo chama kingine kinataka tuwe, ni kuwa na vita hivi vya ndani, na nadhani sio muhimu sana."
Wafuasi wa umma wa Bw Biden wanasema kuchukua nafasi yake kunaweza kuwa faida ya moja kwa moja kwa Warepublican wa Trump, ambao wanaweza kusema kuwa wapinzani wao wamekumbwa na mgogoro ndani ya chama.
"Tunapaswa kuacha kuzungumza juu ya hili," Mwakilishi Debbie Dingell wa Michigan alisema kwenye CNN Jumapili. "Tumetumia wiki nzima. Warepublican wana wakati mzuri. Namaanisha, tunahitaji kurejea kuzungumza kuhusu Donald Trump na utendaji wake."
Je ni njia ya kutaka kumweka Harris?
Mapema wiki hii, aliyekuwa Mwakilishi wa Ohio Tim Ryan aliwasilisha mbele jina la mtu anayeweza kuchukua nafasi ya Biden: Makamu wa Rais Kamala Harris.
"Ninaamini sana kwamba njia yetu bora zaidi ni Kamala Harris," aliandika katika op-ed kwa Newsweek. "Wale wanaosema kuwa mgombea Harris ni hatari kubwa kuliko Joe Biden tuliyemwona usiku mwingine na tutaendelea kuona hawaishi katika ukweli."
Ingawa ameonyesha uungwaji mkono wa dhati kwa Bw Biden, wazo la Bi Harris, 59, kuchukua nafasi ya Bw Biden limepata nguvu katika siku za hivi majuzi.
Katika mahojiano na Adam Schiff Jumapili asubuhi, mbunge huyo alisema Bi Harris anaweza kushinda dhidi ya Trump "kwa wingi".
Kama makamu wa rais, na mgombeaji wa Democrats 2020, wafuasi wanasema tayari amejaribiwa kwa kampeni na anajulikana na taasisi ya Kidemokrasia na wafadhili wake.
Bi Harris "anaijua kazi hiyo", alisema mwenyekiti wa zamani wa Kamati ya Kitaifa ya Democrats Donna Brazile kwenye ABC siku ya Jumapili.
"Kuwaomba wajumbe waliochaguliwa katika kongamano hilo ambao ni wafuasi wa Biden-Harris kumpita Kamala Harris... itakuwa ni utovu wa nidhamu wa kisiasa."

Comments