*VIJANA WA WILAYA YA KIBITI WAHAMASISHWA KUUNDA VIKUNDI NA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI*
Vijana wa Wilaya ya Kibiti,Mkoani Pwani wamehamishwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kupitia vikundi ili kuweza kujiajiri na kupunguza umaskini wa kipato.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira *Mh Anthony Mavunde* wakati akitoa semina kwa kambi la Mafunzo la Vijana wa UVCCM wilaya ya Kibiti kwa kuwataka Vijana wa wilaya ya Kibiti kutumia Rasilimali zilizopo kufanya shughuli za kilimo na uvuvi kupitia vikundi vilivyosajiliwa ili kupunguza changamoto ya ukosefu wa Ajira kwa Vijana.
Aidha wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa UVCCM wa WILAYA *Ndg Juma Ndaruke* na *Charangwa Suleiman* MKOA wa Pwani wameahidi kusaidia uundwaji vikundi vya Vijana ili vijana wa Kibiti wanufaike na fursa za mfuko wa maendeleo wa Vijana.
Akimkaribisha Mgeni Rasmi,Mbunge wa Jimbo la Kibiti *Mh Ally Seif Ungando * ameahidi kusaidia uanzishwaji wa *SACCOS* ya Vijana wa Wilaya ya Kibiti ili Vijana wanufaike na fursa za mikopo na uwezeshwaji.

Comments