ACADEMIC

*[̲̅U̲̅][̲̅N̲̅][̲̅I̲̅] [̲̅G̲̅][̲̅o̲̅][̲̅a̲̅][̲̅l̲̅][̲̅s̲̅]* ๐Ÿ‘จ๐Ÿพ‍๐ŸŽ“๐Ÿ“š๐Ÿ‘ฉ๐Ÿฝ‍๐ŸŽ“



‼‼‼‼‼
*⦅A⦆⦅C⦆⦅A⦆⦅D⦆⦅E⦆⦅M⦆⦅I⦆⦅C⦆  ⦅E⦆⦅X⦆⦅C⦆⦅E⦆⦅L⦆⦅L⦆⦅E⦆⦅N⦆⦅C⦆⦅E⦆ ⦅I⦆⦅N⦆ ⦅U⦆⦅N⦆⦅I⦆⦅V⦆⦅E⦆⦅R⦆⦅S⦆⦅I⦆⦅T⦆⦅Y⦆ *
‼‼‼‼‼


๐Ÿ“š๐Ÿ“š๐Ÿ“š๐Ÿ“š๐Ÿ“š

_Author:_
© *Eng. Mahenge, E.*
๐Ÿ“ฉ *_+255 714 530 295_*

_Editor:_
© *~$#@D3~*
๐Ÿ“ฉ *_+255 683 676 795_*
๐Ÿ“ง *_shadenation95@gmail.com_*
๐Ÿ’Œ *_https://www.instagram.com/shade_nation/_*

_Powered by;_
© *#ฦ’เซจฮตฮต_เซฎษฆฮฑฦญ ๐Ÿค—♥๐Ÿค๐Ÿพ*
๐Ÿ“ฉ *_+255 652 516 048_*
๐Ÿ“ง *_freechatgrp@gmail.com_*
๐Ÿ’Œ *_https://www.instagram.com/freechat_tz/_*

_In Association with;_
© *PFU Group.*
๐Ÿ’Œ *_https://www.instagram.com/prepareforuniversity/_*

๐Ÿ“š๐Ÿ“š๐Ÿ“š๐Ÿ“š๐Ÿ“š





๐ŸŒ *INTRODUCTION:*

*_Definition of terminologies_*

1. Academic (Adjective)

 a. Of or relating to institutionalized education and scholarship, especially at a college or university.

b. Of or relating to studies that rely on reading and involve abstract thought rather than being primarily practical or technical.

c. Relating to scholarly performance

Read more,,,http://www.yourdictionary.com/academic


2. Excellence

- The quality of being outstanding or extremely good.

- Possessing Greatness, Being the very best.

- *_Some Synonyms for Excellence_*

_Beauty, Splendour, Glory, Honour, Mighty, Great, Majestic, Large, Powerful, Wide, Influential, Valuable, Precious, Rare, Head, Top, Summit, Front, Beginning, Strong, Abundance, Leader, Captain, Prince, Commander, Exalted, Rising Up, Magnificent, Extreme, Extraordinary, Very Pre-eminent, Surpassing, Best, Superior, Beyond Measure, Exceeding, Different, Dignity, To Stand out, Prominence, Further, Next._


3. University

- A high-level school offering classes that can lead to a bachelor’s degree, or to master’s and doctoral degrees at the graduate level.

- Institution of higher education (typically accepting students from the age of about 17 or 18, depending on country, but in some exceptional cases able to take younger students) where subjects are studied and researched in depth and degrees are offered.


Nadhani kwa kusoma hizo synonyms tunaona kwa upana namna neno Excellence/Ubora linavyoweza kutazamwa kutokea kona tofauti tofauti. Unaweza kuendelea kutafakari neno moja moja ili uendelee kuona upana wa neno Excellence.


Elimu ya chuo kikuu mara nyingine huitwa elimu ya juu (higher learning), hii hasa ni kwa sababu...

1. Mtu anayesoma level hii ya elimu atafundishwa vitu ambavyo vipo katika level ya juu (professional level) ukilinganisha na level za chini za elimu.

2. Kwa asilimia kubwa, mwanafunzi katika level hii anachukuliwa kuwa ni mtu mzima (adult & matured) kiasi kwamba anajitambua, anajua anataka nini, ana uwezo wa kujisimamia na kutimiza malengo yako. Ndio maana chuo kikuu hakuna kiranja wa kukusimamia.


Kutokana na hili, ubora wa utendaji wako na ufaulu wako pindi uwapo chuoni unakutegemea wewe na jitihada zako kwa zaidi ya asilimia 75.

Kila mtu ana mtazamo wake kuhusu ubora, na mtazamo wako kuhusu ubora ndio utakaoamua approach yako katika masomo pindi uwapo chuo.

Hebu tuangalie baadhi ya mitazamo,,,

1. Kuna wanaotazama ubora kwa kuweza kufaulu masomo kwa kiwango cha juu (GPA kubwa)

2. Kuna wanaotazama ubora kwa kuangalia kiwango chao cha kutendea kazi yale waliyojifunza chuoni, bila kujali GPA inasomaje.

3. Kuna wanaotazama ubora kwa uwezo wa kumaliza chuo na kupata cheti tuu.

4. Kuna wanaotazama ubora kama issue ya ushindani, yaani kuwa wa kwanza darasani, kuwa best student.

5. Kuna wanaotazama ubora kama ni issue binafsi, bila kujali amekuwa wa ngapi darasani, bali ni kwa kiasi gani amefikia malengo yake

So, tuna mtazamo tofauti tofauti, japo kuna umuhimu wa kutengeneza balance ya mitazamo mbali mbali ili uweze kuwa mtu mwenye ubora ambao ni universal.

Kwa mfano...
- Unaweza kuwa best student (wa kwanza darasani), lakini ukawa huna uwezo wa kutendea kazi ulichojifunza, this is not excellence.
- Unaweza kuwa vizuri katika practical, ila ukadisco kwenye masomo kwa sababu ya poor performance, hii pia si excellence.

So, ni lazima kuwe na balance, japo kuwa na kiwango cha juu cha ubora ni lazima uwe vizuri sana katika aspects zote za masomo yako, yaani Good GPA, Good in Practical, Achieving your goals, being at the top in your class etc. Try your best to be good in all important aspects.



๐ŸŒ *EXCELLENCE PRINCIPLES:*

Tuangalie vitu viwili kwenye mada hii ya ubora/excellence

1. Kanuni zinazoleta Ubora
2. Vikwazo vinavyozuia Ubora.

Nianze kwa kusema kwamba, ubora siyo tukio bali ni tabia. Ninachomaanisha ni kwamba, ukitaka kuwa bora katika eneo lolote, fahamu kwamba kuna tabia ambazo lazima ujijengee.

Ubora hauji kwa kufanya jambo mara moja, bali kwa kurudia tena na tena. Mchakato wowote wa kujenga tabia huwa unachukua muda. Vivyo hivyo, ukitaka kuwa mtu bora katika masomo yako, ni lazima ujifunze kufanya mambo yanayohitajika kwa kurudia rudia tena na tena.

Ndiyo maana tunaangalia kanuni za kukuwezesha kuwa mtu bora katika masomo yako. Kanuni ni sheria zinazoongoza eneo fulani la maisha. Ukizifuata unafanikiwa. Ukizivunja zinakuvunja.

So, ninachofundisha hapa ni kanuni ambazo ukijenga maisha yako juu yake basi una uhakika wa kuwa mtu bora, si katika masomo tu bali katika kila nyanja ya maisha.

Karibu tutazame kanuni zifuatazo...


0⃣1⃣  *_Kanuni ya kwanza:_*
*UWEPO WA MALENGO AU KUSUDI.*

Huwezi kuwa mtu bora kama kwanza kabisa hujui ni nini unachotaka.

_You can not attain what you have not defined._

- Ni kwa nini upo chuo?
- Ni kwa nini unasoma kozi unayosoma?
- Unatarajia kuwa mtu gani kwa kusomea hiyo kozi?
- Unatarajia kupata nini kwa kusomea hiyo kozi?

Ni lazima uweze kueleza sababu yako/zako za kuwepo chuo na kusomea hiyo kozi. Ni lazima uweze kueleza ni nini unatarajia kutoka nacho pindi umalizapo masomo yako ya chuoni?

- Je, unataka kuwa na ufaulu wa kiwango gani? (First class, Upper second class, Second class, Pass)
- Je, unataka ukimaliza kusoma hiyo kozi uwe na uwezo wa kufanya vitu gani?

Ubora unaanzia kwenye kusudi na malengo. Andika malengo yako vizuri, na ingia chuoni ukijua ni nini hasa unataka. Plan your way into excellence. Excellent does not come accidentally.


0⃣2⃣  *_Kanuni ya pili:_*
*KUWA NA PASSION (UCHU, SHAUKU) WA KILE UNACHOSOMEA.*

Moyo wako usipohusika katika kile unachosomea, ni vigumu kukifanya kwa ubora.

Hisia za kupenda sana kile unachofanya ndiyo nguvu inayowasukuma wengi kufanya vitu kwa ubora.

Ni vigumu sana kufanya vizuri katika kile usichokipenda. Ni vigumu kufanya vizuri sana kama kozi unayosomea huna upendo nayo.

Wengi hupenda kuchagua kozi za kusoma kwa sababu labda zinalipa, ni rahisi kupata ajira, shinikizo la watu wa karibu,  n.k.

No matter the reason, kama unasomea kozi usiyoipenda, kuna ugumu sana kwa wewe kuwa mtu bora. Put your heart in what you are doing today, or you will get nothing out of it tomorrow.!


0⃣3⃣  *_Kanuni ya tatu:_*
*KUJINYIMA RAHA (GETTING OUT OF YOUR COMFORT ZONE).*

Ni kawaida ya binadamu kupenda raha/comfort. We like to be comfortable, but comfort is an enemy of excellence.

Ubora utakutaka ufanye unachotakiwa kufanya hata kama hujisikii kufanya.

- Kuna wakati itakubidi upunguze masaa ya kulala.
- Kuna wakati itabidi ujinyime kuangalia movies/series.
- Kuna wakati itakubidi ujinyime kuangalia mpira.


Kuna vitu vingi ambavyo ukifanya vinakupa raha, lakini vinakuibia muda ambao ungeutumia kuwekeza ili uwe mtu bora.

Ni lazima uwe na vipaumbele sahihi. Do you want to feel good, or do you want to be excellent? The choice is yours!!!


0⃣4⃣  *_Kanuni ya nne:_*
*BIDII/DILIGENCE.*

_You can't excel at what you don't work hard for._

Ubora ni mtoto wa bidii katika kazi. Bidii ni muunganiko wa juhudi na akili. Ni lazima uhusishe vyote katika kusoma ili uwe mtu bora.

It will demand long hours of studying & high level of mental engagement.

Itahitajika uwe serious na unachokifanya. Hakuna nyota yeyote asiye na ushuhuda wa bidii katika kazi. Tazama akina Christian Ronaldo, Leonel Messi, Usain Bolt na nyota wengine wengi, bidii ndiyo kitu kikubwa wanachofanana.

Katika masomo ni vivyo hivyo, bidii yako ndiyo itakayokutofautisha.

Material hayaingii kichwani na hayaeleweki by osmosis au diffusion, ni lazima uketi chini, usome, utafakari, ujadiliane na wengine n.k...


0⃣5⃣  *_Kanuni ya tano:_*
*SELF-EDUCATION (PERSONAL EFFORTS).*

Kuna mnayojifunza darasani. Kuna unayojifunza binafsi. Excellence will demand that you go an extra mile, and this will only be possible through self-education.

Soma vitabu, sikiliza lectures on YouTube and other sites that relates to your profession.

Usiwekewe mipaka na yale mnayojifunza darasani. Kwa nia ya kufaulu tu, ya darasani yanatosha. But kama nia yako ni kuwa mtu bora, basi lazima ujiongeze sana tu.


0⃣6⃣  *_Kanuni ya sita:_*
*USTAHIMILIVU/ENDURANCE.*

Kuna ugumu katika kutafuta ubora, ni lazima ujifunze kustahimili. Haitoshi kuweka bidii siku moja tu, bali kujenga tabia ya kuwa na bidii kila siku.

_Excellence demands continuity, and continuity demands endurance._

Unaweza ukaweka bidii katika semester ya kwanza ya masomo, na matokeo yasije vizuri. Usikate tamaa, badala yake ongeza bidii huku ukijitathimini kujua kama kuna mahali unakosea

All in all, ukitaka ubora usikatishwe tamaa na chochote. Vikwazo vitakuwepo, ila usiruhusu vikutoe kwenye lengo lako.



Ilikuwa tuangalie vikwazo vinavyozuia ubora, lakini kama umesoma kanuni za ubora nilizokushirikisha hapo juu, basi chochote kitakachokufanya ushindwe kuishi kwa kufuata hizo kanuni ni kikwazo katika maisha yao ya ubora.

Iwe ni kutokujiamini, visingizio, kukosa nidhamu, makundi/marafiki unaoambatana nao, uvivu, kutokujua nini unataka kupata kutokana na masomo yako n.k.



๐ŸŒ *UBORA NJE YA MIPAKA YA CHUO (Taking Excellence beyond the academic realm).*


Kuna vitu unapaswa kujifunza pindi uwapo chuoni na vikakusaidia hadi utakapotoka kwenye mazingira ya chuo na kwenda sehemu yoyote katika maisha.

Kuna kanuni ambazo zimefichwa katika mfumo wa elimu, ni kanuni muhimu sana ambazo zitakufanya uwe na ubora katika maisha kama tu utazifahamu na kuzifuata.

Napenda ufahamu kwamba, mfumo wa elimu haukutengenezwa ili kukufundisha taaluma yako tu, bali pia kwa ajili ya kukufundisha kanuni za muhimu zinazotawala katika maisha.

Lengo la ubora katika masomo ni kuwa bora katika maisha.

_We want to be excellent in our studies so that we can be excellent in life._

So, tutakwenda kuona kanuni za muhimu zilizofichwa katika mfumo au mifumo ya elimu, na ambazo lengo lake kubwa ni kukufundisha maisha na namna unavyopaswa kuenenda ili uwe mtu bora katika maisha.


1⃣ *UWEPO WA KUSUDI.!*

Hakuna taasisi yoyote ya elimu ambayo utaona imeanzishwa bila kuwepo kwa kusudi la kuanzishwa.

Shule za msingi zipo kwa ajili ya kuweka msingi.

Shule za secondary zipo kwa ajili ya kutengeneza nguzo.

Vyuo vya ufundi vipo kwa ajili ya kukupa ujuzi.

Vyuo vikuu vipo kwa ajili ya kukukamilisha katika taaluma fulani.

Kuna vyuo vya uhandisi na vyuo vya biashara na vyuo vya diplomasia n.k.

Hakuna chuo chochote kinachoanzishwa bila kuwa na kusudi la kuanzishwa. Ndio maana kila chuo utaona kila vision na mission statements. Pia katika chuo, kila kozi inayotolewa ina makusudi yake. They call it Course Objectives.

Uwepo wa kusudi ni jambo la muhimu sana katika ngazi au taasisi yoyote ya elimu.

Hii inatufundisha kuwa hakuna kilichopo kwenye maisha kisicho na kusudi. Wewe binafsi una kusudi la kuwepo. Pia unapaswa kuwa na kusudi katika kila jambo unalofanya au unalotaka kufanya katika maisha.

Tunapitishwa katika ngazi mbalimbali za elimu zenye makusudi fulani ili tujifunze kutofanya mambo bila kuwa na kusudi la kuyafanya. Pia tunajifunza kwamba hata maisha yetu yana sababu na kusudi la kuwepo.


2⃣ *UWEPO WA MITALAA/CURRICULUM.!*

Hakuna chuo kisicho na mtalaa wa kuongoza uendeshaji wa masomo. Vilevile  hakuna ngazi ya elimu isiyokuwa na curriculum inayoeleza kwa wazi ni nini hasa kitakuwa kinafundishwa na ni kwa namna gani kitafundishwa.

Hakuna kozi inayotolewa bila kuwepo kwa curriculum iliyoandikwa na kuidhinishwa. Kwa mfano, Kama chuoni unasomea Business Administration, basi ni lazima iwepo curriculum husika kwa ajili ya kozi hiyo. Na kila chuo kinakuwa na curriculum yake inayojitegemea.


Mfumo wa elimu upo hivyo ili kutufundisha kwamba, haitoshi tu kujua unachotaka kutimiza katika maisha, bali unapaswa kujua ni kwa namna gani utatimiza na uweke katika maandishi mbinu na zana utakazotumia ili kutimiza.

Sote tunapaswa kutengeneza mfumo katika maandishi ambao utatumika kama ramani ya kutuongoza kutimiza malengo na makusudi tuliyonayo.

_Do you have a curriculum of your life?_



3⃣ *UWEPO WA RATIBA / TIME LIMIT.!*

Hakuna chuo chochote duniani ambacho kinatoa mafunzo bila kuyawekea muda. Utaambiwa, kozi yako itachukua miaka miwili, au mitatu au minne n.k

Pia, utakuta kozi imegawanywa kwa semester mbalimbali, na kila somo katika kozi limepewa masaa kadhaa ya kutumika katika kufundisha. Hivi vitu havijawekwa kwa bahati tuu, kuna kanuni zilizotumika kuhakikisha kila kitu kinawekewa mipaka ya muda.

_Unadhani kwanini katika masomo kuna ratiba inayoeleweka?_

Imagine ungekuwa unaingia chuo na hujui ni lini utamaliza...

Hii itufundishe kwamba, kama ambavyo tunabanwa na muda pindi tuwapo masomoni, vivyo hivyo katika maisha tunapaswa kujibana kwenye muda.

Shule inatufundisha kuendesha maisha yetu kwa ratiba.

Shule inatufundisha kwamba, hakuna kitu cha kufanya milele, unapoanza kufanya kitu jaribu kupiga mahesabu ya muda na kujiwekea time limit ya kumaliza shughuli zako.

Ratiba tunazofuatwa mashuleni au vyuoni hazikuwekwa ili tu kutubana, bali ili kutufundisha kwamba hivi ndivyo maisha yanavyopaswa kuendeshwa.

_Je, unaendesha maisha yako kwa ratiba?_



4⃣ *UWEPO WA MITIHANI (ASSIGNMENTS, QUIZZES, EXAMS).!*

Kwa nini wameweka mitihani vyuoni au mashuleni?

Ni lazima tufahamu kwamba kazi ya shule au chuo ni kukuandaa kwa ajili ya maisha na siyo kwa ajili ya kufaulu. Kila kinachofanyika chuoni kinakuandaa kwa ajili ya maisha.

So, hata mitihani tunayofanya katika mifumo ya elimu, siyo tu kwa ajili ya kutupima uelewa wetu, bali pia kwa ajili ya kutujengea mtazamo sahihi kuhusu maisha.

Kama ambavyo tunakutana na mitihani katika masomo, vivyo hivyo tutakutana na mitihani katika maisha.

Kama ambavyo unajiandaa na kutumia akili ili kukabiliana na mitihani uwapo masomoni, vivyo hivyo unapaswa kujiandaa na kutumia akili katika kukabiliana na mitihani na changamoto za maisha.

Ukipiga chabo kwenye mitihani shuleni, unajitengenezea mentality ya kutafuta shortcut katika maisha. Ukitaka kufaulu kwa njia zisizo halali, unajitengenezea mentality ya kwamba katika maisha unaweza kutoka hata kwa njia zisizo halali.

Tafadhali, fahamu kwamba lengo siyo kufaulu tu bali kujijengea stamina ya maisha. Tumia muda uwapo chuoni na kila unachofanya chuoni kwa ajili ya kujijengea mtazamo sahihi kuhusu maisha.



5⃣ *UWEPO WA WALIMU (LECTURERS, TUTORS, PROFESSORS).!*

Wanafunzi hawajifundishi chuoni, bali wanakuwa chini ya uongozi na usimamizi wa walimu.

Kuna kitu unatamani kujua, kuna ujuzi unataka kuupata, but ni lazima ukubali kuwa chini ya mtu anayejua kile usichokijua ili uweze kujifunza.

Hii ni kanuni ya muhimu sana katika maisha.

Kuna vitu unatamani kuwa navyo katika maisha, lakini vitu hivyo vipo mikononi mwa watu wengine. Kuna vitu unatamani kufanya katika maisha, lakini kuna watu waliokutangulia ambao wapo kwenye nafasi ya kukufunza.

Jifunze kunyenyekea, jifunze kutafuta msaada, tafuta kujifunza kwa wengine. Usihangaike kutafuta njia yako wakati kuna watu wanaifahamu njia tayari na wanaweza kukufundisha.

Elimu inatufundisha kwamba tunahitajiana. Kuna wakati  mtu mzima anafundishwa na mwalimu mwenye umri wa mtoto wake, lakini ndivyo ilivyo, ukiwa na uhitaji jifunze kunyenyekea kwa walio katika nafasi ya kukusaidia.

_Be humble enough to learn from others, no matter your title or age.!_


Nimejaribu kukuonyesha mfano kwa kutumia hizo points tano, lakini basically katika kila unachofanya pindi uwapo chuoni kina implication yake katika maisha. Hiki ndicho nilichogundua kwa kutafakari kwangu kuhusu mfumo mzima wa elimu jinsi ulivyotengenezwa.

So mimi nimekuanzishia, wewe unaweza kwenda mbele zaidi kwa kuangalia mambo mengine mengi yaliyomo kwenye mifumo ya elimu na implication yake katika maisha.

Kwa mfano...
- Kwa nini kuna kulipa ada vyuoni au shuleni?
- Kwa nini kuna adhabu na uhitaji wa nidhamu?
- Kwa nini kuna kufeli na kufaulu?
- Kwa nini kuna kusoma, kuandika, kuchora?
- Kwa nini kuna uwepo wa uongozi wa wanafunzi?

Na mengine mengi unayoweza kukutana nayo pindi uwapo chuoni. Jifunze kuuliza umuhimu wa kila unachofanya chuoni katika maisha yako ya sasa na ya baadaye. Ukijijengea tabia hii, utajifunza principles nyingi sana za kukusaidia katika maisha.

Haya mambo nayaandalia kitabu, Mwenyezi Mungu akijalia mwishoni mwa mwaka huu au 2019 mwanzoni ili kuweza kuwasaidia wanafunzi ku-maximize fikra zao wawapo chuoni.

Otherwise, nilipenda kuonyesha kwamba lengo la kutaka kuwa excellent in your academics ni ili uwe excellent in life.

_We must build in ourselves the capacity to translate our academic excellence into life excellence._

_You are great people, and I believe in you. No matter where you are and no matter your background, you can be an example of how excellence looks like._

_I wish you all the best brothers and sisters!_




```Tafadhali, usisite kuwashirikisha ndugu, jamaa pamoja na marafiki zako pia. Ahsante sana!!!```
๐Ÿค—♥๐Ÿค๐Ÿพ

Comments